BREAKING...... KIMENUKA KOREA NA MAREKANI
MNDEME BLOG Korea Kaskazini imesema kuwa inaweza kuahirisha mpango wa kiongozi wake, Kim Jong-un kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump kutokana na matamko pamoja na mazoezi ya kijeshi ya pamoja yanayofanywa kati ya Marekani na Korea Kusini. Kupitia tamko lililotolewa na Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, nchi hiyo imelaani kauli zilizotolea na Mshauri wa Mambo ya Ulinzi wa Marekani, John Bolton dhidi yake. Aliielezea kauli ya Bolton aliposikika akidai kuwa Korea Kaskazini inaweza kufuata nyayo za Libya katika kuachana na mpango wa silaha zake kuwa ni kutaka kufananisha hatma ya taifa hilo na ile ya Libya iliyokuwa ikiongozwa na Muammar Gaddafi au Iraq ya Saddam Hussein. “Ni jambo lisilokubalika na hatua mbaya kutaka kuingiza hisia za hatma ya Libya au Iraq, mataifa ambayo yalianguka kutokana na jitihada za kutaka kuharibu nguvu za nchi hizo,” imeeleza taarifa hiyo. Aidha, Korea Kaskazini pia imesema kuwa inashangazwa na kauli za Marekani kuita