NGUVU YA DHAIFU SEHEMU 1&2 RIWAYA YA KUSISIMUA, NISIMULIZI YA KWELI SIKUJUWA ISOME HAPO
MNDEME BLOG Mamaaa” Aliniita Kareen kwa sauti ya kustua sana. Ndani ya sekunde chache akili iliwaza mambo kama kumi hivi kwa hofu. Geofrey mume wangu akanitazama, “Usiwe unastuka sana, kelele kwa watoto ni kawaida.” Nilimpuuza na kuinuka mbio kuelekea kule nje walikokuwa wanacheza watoto. Ni kawaida kwa mtoto kuita hivyo, lakini sijui kwanini siku hiyo nilistuka sana. Ni kama nafsi yangu ilijua kuna kitu kimetokea. Ni kweli kuna kitu kilikua kimetokea, tena kitu kikubwa haswaa. Baada ya ndoa sikupata mtoto mara moja. Niliolewa umri ukiwa umeenda kidogo tofauti labda na rafiki zangu wengi au ndugu zangu wengine. Ingawa mimi sikuona kama ni jambo baya au huenda sikujiona nimechelewa sana, ila kutokana na walionizunguka nilihisi nitatakiwa kupata mtoto mara tu nitakapoingia kwenye ndoa. Unajua mara nyingi matatizo tunayokuwa nayo katika maisha huwa hasa matatizo kwa ajili ya jamii inayotuzunguka. Yaani mfano mtu anayemaliza shule akakutana na changamoto ya kupata kazi, w