ABDUL NONDO AMKATAA HAKIMU
MNDEME BLOG Mshtakiwa katika kesi ya kujiteka na kusambaza taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, Abdul Nondo ameandika barua ya kumkataa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, John Mpitanjia, anayesikiliza kesi hiyo kwa madai ya kuwa karibu na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Iringa. Wakili anayemtetea Nondo, Jebra Kambole ametoa sababu tano za mteja wake kuandika barua hiyo tangu Mei 11, mwaka huu za kumkataa hakimu huyo ikiwamo hakimu huyo kuonekana akiingia katika gari la Mkuu wa Upelelezi na kwenda sehemu isiyojulikana, ambapo kutokana na hali hiyo, mteja wake ameona haki haitatendeka. Amedai sababu nyingine ni hakimu huyo kukutwa amekaa na Paul Kisapo ambae ni shahidi wa tatu katika kesi hiyo. Kwa upande wake Wakili Upande wa Jamhuri, Abel Mwandalama amedai pamoja na kupokea barua ya mshtakiwa kumkataa hakimu lakini ameona hayana msingi katika kesi hiyo. “Tunasema hayo kwa kuwa Aprili 19, shahidi wa tatu katika shauri hilo alitoa ushahid