Posts

BREAKING...... KIMENUKA KOREA NA MAREKANI

Image
MNDEME BLOG   Korea Kaskazini imesema kuwa inaweza kuahirisha mpango wa kiongozi wake, Kim Jong-un kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump kutokana na matamko pamoja na mazoezi ya kijeshi ya pamoja yanayofanywa kati ya Marekani na Korea Kusini. Kupitia tamko lililotolewa na Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, nchi hiyo imelaani kauli zilizotolea na Mshauri wa Mambo ya Ulinzi wa Marekani, John Bolton dhidi yake. Aliielezea kauli ya Bolton aliposikika akidai kuwa Korea Kaskazini inaweza kufuata nyayo za Libya katika kuachana na mpango wa silaha zake kuwa ni kutaka kufananisha hatma ya taifa hilo na ile ya Libya iliyokuwa ikiongozwa na Muammar Gaddafi au Iraq ya Saddam Hussein. “Ni jambo lisilokubalika na hatua mbaya kutaka kuingiza hisia za hatma ya Libya au Iraq, mataifa ambayo yalianguka kutokana na jitihada za kutaka kuharibu nguvu za nchi hizo,” imeeleza taarifa hiyo. Aidha, Korea Kaskazini pia imesema kuwa inashangazwa na kauli za Marekani kuita

UPDATE, MBUNGE WA CCM ALIA BUNGENI INGIA KUSOMA ZAIDI

Image
MNDEME BLOG Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Jacqueline Ngonyani  ‘Msongozi’ ametoa chozi bungeni akiitaka Serikali kuwalipa mawakala wa pembejeo na kuacha kutumia kivuli cha uhakiki wa madeni hayo kutoyalipa. Akichangia bajeti ya kilimo, leo Mei 15, 2018 bungeni, Msongozi amesema madai hayo yamedumu kwa zaidi ya miaka minne huku baadhi wakifariki kabla hawajalipwa. “Nashangaa sana mawakala wa pembejeo wanadai miaka minne, walihudumia wakulima wetu na walikwenda kukopa fedha katika taasisi, ambazo sasa zinawadai,” amesema Msongozi. Huku akishangiliwa na wabunge, Msongozi amesema, “Serikali imekuwa inajificha katika kichaka cha uhakiki, kwa nini hawawalipi? Serikali imekwenda kujificha katika uhakiki, ni uhakiki wa aina gani? Kuna watu wanakufa bila kupewa fedha zao.” Msongozi akizungumza kwa sauti yenye kuashiria kulia huku mkono wake akiupeleka kufuta uso wake, amesema, “katika nchi hii watu wanatafuta haki zao, kama wameiba kwa nini wasipelekwe mahakamani, kwa nini hawa

ABDUL NONDO AMKATAA HAKIMU

Image
MNDEME BLOG Mshtakiwa katika kesi ya kujiteka na kusambaza taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, Abdul Nondo ameandika barua ya kumkataa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, John Mpitanjia, anayesikiliza kesi   hiyo kwa madai ya kuwa karibu na Mkuu wa Upelelezi wa  Polisi Mkoa wa Iringa. Wakili anayemtetea Nondo,  Jebra Kambole ametoa sababu  tano za mteja wake kuandika barua hiyo tangu Mei 11,  mwaka huu za kumkataa hakimu huyo ikiwamo hakimu huyo kuonekana akiingia katika gari la Mkuu wa Upelelezi na kwenda sehemu isiyojulikana, ambapo kutokana na hali hiyo, mteja wake ameona haki haitatendeka. Amedai sababu nyingine ni hakimu huyo kukutwa amekaa na Paul Kisapo ambae ni shahidi wa tatu katika kesi hiyo. Kwa upande wake Wakili Upande wa Jamhuri, Abel  Mwandalama amedai pamoja na kupokea barua ya mshtakiwa kumkataa hakimu lakini ameona hayana msingi katika  kesi  hiyo. “Tunasema hayo kwa kuwa Aprili 19, shahidi wa tatu katika shauri hilo alitoa  ushahid

BREAKING NEWS SUGU ATOKA GERENZANI MBEYA.

Image
MNDEME BLOG Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ameachiwa huru leo Mei 10, 2018 kutoka katika Gereza la Ruanda jijini Mbeya alikokuwa amefungwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, amefunguka na kuweka wazi kilichojiri. Amesema hakuwa anafahamu iwapo angeachiwa huru leo hadi polisi walipomfuata na kumwambia ajiandae. Amedai mapaka sasa hafahamu imekuwaje hadi akaachiwa kwani ilijulikana ataachiwa Juni 5, ambapo kifungo chake kingekamilika. “Watu wote walitarajia ningetoka jela mwezi Juni, lakini ghafla jana niliambiwa nijiandae kwamba kesho asubuhi (leo) natakiwa niachiwe huru, nilipotoka nje nikakuta askari wengi, nikaelekezwa kuingia kwenye gari la RCO mimi na mwenzangu Masonga, tukasindikizwa na maofisa magereza watano hadi nyumbani na kutukabidhi kwa familia. “Watu wanauliza, imekuwaje? Lakini mimi ninawaambia sijui, kwa sababu haikuwa kazi yangu kufanya hesabu za magereza, hiyo ni kazi ya magereza, kwa sababu mimi ninacho

BREAKING KUTOKA LOAN BOARD INGIA KUAAPPLY MKOPO

Image
MNDEME BLOG  Click bellow to apply students loan for 2018/19       APPLY LOAN HERE New oudo #shampoo swagga. Gusa alama ya download hapo chini ili uweze kupakua wimbo mzuri kutoka kwa shampoo music Usisahau kushare blog hii, au tutafute kwa sim no. 0652530530

BREAKING NEWS MAHAKAMA YATOA HUKUMU KESI YA NABII TITO

Image
MNDEME BLOG Mahakama  ya Wilaya ya Dodoma, imemfutia mashtaka ya kutaka kujiua na kuamuru akapatiwe matibabu ya afya ya akili katika Taasisi ya Mirembe Isanga, mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma, Onesmo Machibya (44), maarufu kama ‘Nabii Tito’. Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kupokea ripoti za vipimo vya afya ya akili ya Nabii Tito kutoka Mirembe Isanga, vinavyothibitisha kuwa ana ugonjwa wa akili. Awali, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Kalayemaha, aliagiza kuwa Nabii Tito apelekwe katika taasisi hiyo ya magonjwa ya akili ili kupatiwa matibabu ya afya ya akili na mahakama imemwondelea mashitaka yaliyokuwa yakimkabili. Alisema katika ripoti ya kitabibu inaonyesha kuwa Nabii Tito kweli ana matatizo ya afya ya akili, hivyo anatakiwa kupelekwa katika taasisi hiyo ya Isanga Mirembe ili kupatiwa matibabu. Mahakama hiyo, Februari 5, mwaka huu, iliamuru kuwasilishwa kwa vielelezo vinavyoonesha Nabii Tito ana matatizo ya akili na kufanyiwa

DOWNLOAD NYIMO MPYA 6 ZA JAHAZI MODERN TAARAB

Image
MNDEME BLOG Gusa hapo chini ili uweze kudownload ngoma kali za jahazi 6 kwenye single moja. Usisahau kushare na kukomenti blog hii ili uwe wa kwanza kupata ngoma zote mpya. Tutafute kwa sim no. +255652530530 whtasp kama unahitaji tukusambazie wimbo wako free.