SUGU AKILIPUA TENA BUNGENI EBU SOMA HAPO
MNDEME BLOG Leo May 21, 2018 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesimama na kuuliza swali Bungeni kwa mara ya kwanza tangu atoke gerezani Ruanda, Mbeya May 10 alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano. Sugu aliuliza swali lake mara baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) lililohusu sheria za makosa ya mtandao. Mwenyekiti wa Bunge, Chenge alimruhusu Sugu aulize swali la nyongeza ambapo alisema: “Ahsante Mheshimiwa Mwenyekiti, niwatakie mfungo mwema ndugu zangu Waislamu, ndani ya bunge na nchi nzima kwa wale ambao ni viongozi wautumie mwezi huu kujitathmini. Kutokana na maelezo hayo ya Sugu, Chenge alimkatisha Sugu na kumtaka kuuliza swali moja kwa moja. Sugu aliendelea kwa kusema: “Sheria hii pamoja na sheria nyingine mbovu za habari si tu zinawabana wananchi kupata habari bali zinatumika pia kufunga watu jela hovyo kisiasa… “Mfano mimi nilifungwa kw