Posts

DOWNLOAD NEW OUDIO SHAMPOO| BABY DANCE

Image
MNDEME BLOG Download new oudio from Shampoo  DOWNLOAD OUDIO Kwa matangazo na mengineyo tutafute kwa sim no. 0652530530

SUGU AKILIPUA TENA BUNGENI EBU SOMA HAPO

Image
MNDEME BLOG Leo May 21, 2018 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesimama na kuuliza swali Bungeni kwa mara ya kwanza tangu atoke gerezani Ruanda, Mbeya May 10 alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano. Sugu aliuliza swali lake mara baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa  kujibu swali la msingi la  Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) lililohusu sheria za makosa ya mtandao. Mwenyekiti wa Bunge, Chenge alimruhusu Sugu aulize swali la nyongeza ambapo alisema: “Ahsante Mheshimiwa Mwenyekiti, niwatakie mfungo mwema ndugu zangu Waislamu, ndani ya bunge na nchi nzima kwa wale ambao ni viongozi wautumie mwezi huu kujitathmini. Kutokana na maelezo hayo ya Sugu, Chenge alimkatisha Sugu na kumtaka kuuliza swali moja kwa moja. Sugu aliendelea kwa kusema: “Sheria hii pamoja na sheria nyingine mbovu za habari si tu zinawabana wananchi kupata habari bali zinatumika pia kufunga watu jela hovyo kisiasa… “Mfano mimi nilifungwa kw

BAD NEWS, MWANZA MWANAFUNZI AFARIKI KWA AJALI YA KURIPUKIWA

Image
MNDEME BLOG Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Sabasaba jijini Mwanza, Dotto Baraka (13) amefariki dunia baada ya kulipukiwa na betri ya simu aliyokuwa akiiunganisha na radio chakavu. Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo ambapo amesema limetokea Mei 17, mtaa wa Igoma Mashariki jijini Mwanza. “Baada ya kutoka shuleni, marehemu akiwa na watoto wenzake alianza kutengeneza radio chakavu kwa kuchukua betri ya simu na kuunganisha kwenye nyanya za radio hiyo akitumia mdomo ndipo mlipuko ulipotokea na kusababisha kifo chake," amesema Kamanda Msangi. Aidha Kamanda Msangi ameongeza kuwa wakati tukio hilo linatokea, wazazi wa watoto hao walikuwa safarini huko wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Hata hivyo katika tukio hilo hakuna mtoto mwingine aliyejeruhiwa.Endelea kuwafuatilia mndeme blog kila siku

BREAKING...... KIMENUKA KOREA NA MAREKANI

Image
MNDEME BLOG   Korea Kaskazini imesema kuwa inaweza kuahirisha mpango wa kiongozi wake, Kim Jong-un kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump kutokana na matamko pamoja na mazoezi ya kijeshi ya pamoja yanayofanywa kati ya Marekani na Korea Kusini. Kupitia tamko lililotolewa na Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, nchi hiyo imelaani kauli zilizotolea na Mshauri wa Mambo ya Ulinzi wa Marekani, John Bolton dhidi yake. Aliielezea kauli ya Bolton aliposikika akidai kuwa Korea Kaskazini inaweza kufuata nyayo za Libya katika kuachana na mpango wa silaha zake kuwa ni kutaka kufananisha hatma ya taifa hilo na ile ya Libya iliyokuwa ikiongozwa na Muammar Gaddafi au Iraq ya Saddam Hussein. “Ni jambo lisilokubalika na hatua mbaya kutaka kuingiza hisia za hatma ya Libya au Iraq, mataifa ambayo yalianguka kutokana na jitihada za kutaka kuharibu nguvu za nchi hizo,” imeeleza taarifa hiyo. Aidha, Korea Kaskazini pia imesema kuwa inashangazwa na kauli za Marekani kuita

UPDATE, MBUNGE WA CCM ALIA BUNGENI INGIA KUSOMA ZAIDI

Image
MNDEME BLOG Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Jacqueline Ngonyani  ‘Msongozi’ ametoa chozi bungeni akiitaka Serikali kuwalipa mawakala wa pembejeo na kuacha kutumia kivuli cha uhakiki wa madeni hayo kutoyalipa. Akichangia bajeti ya kilimo, leo Mei 15, 2018 bungeni, Msongozi amesema madai hayo yamedumu kwa zaidi ya miaka minne huku baadhi wakifariki kabla hawajalipwa. “Nashangaa sana mawakala wa pembejeo wanadai miaka minne, walihudumia wakulima wetu na walikwenda kukopa fedha katika taasisi, ambazo sasa zinawadai,” amesema Msongozi. Huku akishangiliwa na wabunge, Msongozi amesema, “Serikali imekuwa inajificha katika kichaka cha uhakiki, kwa nini hawawalipi? Serikali imekwenda kujificha katika uhakiki, ni uhakiki wa aina gani? Kuna watu wanakufa bila kupewa fedha zao.” Msongozi akizungumza kwa sauti yenye kuashiria kulia huku mkono wake akiupeleka kufuta uso wake, amesema, “katika nchi hii watu wanatafuta haki zao, kama wameiba kwa nini wasipelekwe mahakamani, kwa nini hawa

ABDUL NONDO AMKATAA HAKIMU

Image
MNDEME BLOG Mshtakiwa katika kesi ya kujiteka na kusambaza taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, Abdul Nondo ameandika barua ya kumkataa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, John Mpitanjia, anayesikiliza kesi   hiyo kwa madai ya kuwa karibu na Mkuu wa Upelelezi wa  Polisi Mkoa wa Iringa. Wakili anayemtetea Nondo,  Jebra Kambole ametoa sababu  tano za mteja wake kuandika barua hiyo tangu Mei 11,  mwaka huu za kumkataa hakimu huyo ikiwamo hakimu huyo kuonekana akiingia katika gari la Mkuu wa Upelelezi na kwenda sehemu isiyojulikana, ambapo kutokana na hali hiyo, mteja wake ameona haki haitatendeka. Amedai sababu nyingine ni hakimu huyo kukutwa amekaa na Paul Kisapo ambae ni shahidi wa tatu katika kesi hiyo. Kwa upande wake Wakili Upande wa Jamhuri, Abel  Mwandalama amedai pamoja na kupokea barua ya mshtakiwa kumkataa hakimu lakini ameona hayana msingi katika  kesi  hiyo. “Tunasema hayo kwa kuwa Aprili 19, shahidi wa tatu katika shauri hilo alitoa  ushahid

BREAKING NEWS SUGU ATOKA GERENZANI MBEYA.

Image
MNDEME BLOG Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ameachiwa huru leo Mei 10, 2018 kutoka katika Gereza la Ruanda jijini Mbeya alikokuwa amefungwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, amefunguka na kuweka wazi kilichojiri. Amesema hakuwa anafahamu iwapo angeachiwa huru leo hadi polisi walipomfuata na kumwambia ajiandae. Amedai mapaka sasa hafahamu imekuwaje hadi akaachiwa kwani ilijulikana ataachiwa Juni 5, ambapo kifungo chake kingekamilika. “Watu wote walitarajia ningetoka jela mwezi Juni, lakini ghafla jana niliambiwa nijiandae kwamba kesho asubuhi (leo) natakiwa niachiwe huru, nilipotoka nje nikakuta askari wengi, nikaelekezwa kuingia kwenye gari la RCO mimi na mwenzangu Masonga, tukasindikizwa na maofisa magereza watano hadi nyumbani na kutukabidhi kwa familia. “Watu wanauliza, imekuwaje? Lakini mimi ninawaambia sijui, kwa sababu haikuwa kazi yangu kufanya hesabu za magereza, hiyo ni kazi ya magereza, kwa sababu mimi ninacho