Posts

TAARIFA KAMILI YA JESHI LA POLICE MOROGORO KUHUSU KIFO CHA DIWANI WA CHADEMA KILOMBELO

Image
MNDEME BLOG Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema mauaji ya diwani wa kata ya Namwawala kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godfrey Luena huenda yametokana na ulipizaji kisasi wa mauaji ya mwaka 2016. Luena aliuawa juzi usiku baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake wilayani Kilombero. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema jana kuwa watu wasiojulikana walizima umeme nyumbani kwake na kumvamia kwa mapanga na kwamba baada ya mauaji hayo hawakuchukua kitu chochote. “Marehemu amejenga pembezoni kidogo ya msitu," alisema Kamanda Matei. "Baada ya mauaji watu hao walikimbilia msituni". "Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi na kiini cha tukio hili Jeshi la Polisi linasema ni kisasi. Baada ya wauaji hawakuchukua kitu chochote.” Kamanda Matei alisema taarifa za awali zinahusisha kifo hicho na kile cha mkazi mwingine wa Namwawala, Keenan Haule, kilichohusishwa na ushahidi na mgogoro wa mashamba

FULL STORY KUHUSU SHAMBULIZI LA DIWANI WA CHADEMA KILOMBELO, Ingia kuona vedeo

Image
MNDEME BLOG https://youtu.be/kDE_oXONNT0

INASIKITISHA INGIA HAPA KISHA GUSA LINK HAPO CHINI KUONA VIDEO YA MAREHEMU AKWILINA MUDA MCHACHE KABLA YA KIFO CHAKE

Image
https://youtu.be/9kVdEAMzpjI

TAARIFA KAMILI KUHUSU KUPIGWA RISASI MWANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ..............

Image
MNDEME BLOG Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kimesema aliyepigwa risasi jana Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam na kufariki dunia ni mwanafunzi wa chuo hicho. Chuo hicho kimemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Akwilina Akwiline aliyekuwa anasoma shahada ya kwanza ya ununuzi na ugavi. Leo, Februari 17, 2018, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandamana jana. Wafuasi hao wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliandamana kuelelea ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.  Aidha Ofisa Uhusiano wa NIT, Ngasekela David amesema wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha wanafunzi huyo. "Ni kweli alikuwa wanafunzi wetu na tumepokea kwa masikitiko taarifa hizi. Tunaendelea kufuatilia zaidi, "amesema David. Hatahivyo mwanafunzi

BASHE WA CCM AIUNGA MKONO CHADEMA KINONDONI...... Soma zaidi...

Image
MNDEME BLOG Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameungana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kulaani tukio la kikatili lililomtokea Katibu wa CHADEMA Kata ya Hananasif, Daniel John siku za hivi karibuni. Bashe ametoa kauli hiyo katika jukwaa la CCM wakati akimuombea ridhaa mgombea wao Maulid Mtulia ili aweze kuwa muwakilishi wa Jimbo la Kinondoni katika siku zijazo endapo atapata kura nyingi za ndio siku ya kupiga kura ambapo mpaka sasa zimebakia takribani siku mbili. "Naviomba vyombo vya ulinzi na usalama, vifanye kila jitihada kufanya uchunguzi wa kina ili aliyefanya uhalifu huu aweze kupatikana. Kumekuwa na tabia kila uchaguzi mdogo unapofanyika matendo ya kihalifu hufanyika halafu wenzetu wa upande wa pili huamishia kesi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)", amesema Bashe. Pamoja na hayo, Bashe ameendelea kwa kusema "jambo hili lililotokea Jimbo la Kinondoni ni kulaaniwa, sisi tunalilaani na nyie wananchi wa Kinondoni muendelee kul

JIJINI MWANZA, KIWANJA KINAUZWA, NYUMBA NA VYUMBA VINAKODISHWA ingia kwa link kusoma zaidi

Image
MNDEME BLOG Mwanzaaaa are you readyyyyyyyyyyy.......... Kutana na dalali maarufu update Nyumba ya kupanga, chumba, chumba na sebule, nyumba ya kununua na kiwanja. Kunaoffa ya kiwanja nipo isamilo mji mwema bei maelewano wasiliana kwa sim no 0652 530 530. Kuna nyumba inapangushwa, chumba pamoja na chumba na sebule, vyote vipo isamilo mjimwema Katika Jiji la Kwanza na wasiliana na sim no. 0652530530.

B R E A KING N E W S..... JAJI MKUU AIONYA SERIKALI DHIDI YA KUWABANA WAPINZANI....... Soma zaidi chini ya link.

Image
MNDEME BLOG   Jaji Mkuu nchini Kenya David Maraga, ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi hiyo katika kukabiliana na upinzani.  Jaji Maraga ametoa kauli hiyo ikiwa imepita masaa kadhaa tokea kufukuzwa kwa mwanasheria maarufu ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia kuapishwa Raila Odinga katika uwanja wa ‘Uhuru Park’ kufukuzwa nchini humo na kupelekwa Canada. Katika ukurasa wake wa Twitter Jaji Maraga amesema malalamiko yaliyopelekwa Mahakamani yalikuwa wazi na majukumu ya kufanyia maamuzi yalikuwa ya Mahakama kutokana na kwamba ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe. Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya Kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama.  Endelea kufuatilia blog yetu kwa matangazo na biashara tuma msg 0662530530.