TAARIFA KAMILI KUHUSU KUPIGWA RISASI MWANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ..............

MNDEME BLOG
Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kimesema aliyepigwa risasi jana Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam na kufariki dunia ni mwanafunzi wa chuo hicho.

Chuo hicho kimemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Akwilina Akwiline aliyekuwa anasoma shahada ya kwanza ya ununuzi na ugavi.

Leo, Februari 17, 2018, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandamana jana.

Wafuasi hao wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliandamana kuelelea ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho. 
Aidha

Ofisa Uhusiano wa NIT, Ngasekela David amesema wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha wanafunzi huyo.

"Ni kweli alikuwa wanafunzi wetu na tumepokea kwa masikitiko taarifa hizi. Tunaendelea kufuatilia zaidi, "amesema David. Hatahivyo mwanafunzi huyo alikuwa safarini kuelekea bagamoyo kwaajili ya kuomba nafasi ya mafunzo kwa vitendo.
Mndeme blog tunatoa pole kwa wazazi, walezi, mwanafunzi wenza pamoja na jamii kwa ujumla kwa tukio la kushtusha la kifo cha mwanafunzi.

Comments

Popular posts from this blog