MNDEME BLOG Maandamano ya aina yoyote ni haki ya mwananchi na yanaruhusiwa kisheria lakini maandamano hayo lazima yafuate sheria na taratibu zilizobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria ya maandamano inamtaka mwananchi au kundi la wananchi wanaohitaji kufanya maandamano kutoa taarifa kwa maandishi kwa Mkuu wa Polisi wa eneo husika kabla ya masaa 48 ya kuanza kwa maandamano hayo ikieleza dhumuni la maandamano hayo. Pia wahusika wanatakiwa wawe tayari kwa jibu lolote kutoka kwa mkuu huyo kwa kuwa chochote watakachojibiwa lazima kiwe na sababu. Endapo wahusika watakataliwa kufanya maandamano na hawatoridhishwa na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Polisi kuna hatua mbili muhimu zinazotakiwa kufuatwa na sio wahusika kujiamulia kuandamana kilazima kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa. Hatua hizo muhimu zinazotakiwa kufuatwa ni kuandika barua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kumueleza kutoridhishwa na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Polisi ili ...
MNDEME BLOG MPATAKUVA , MZUNGWA NA MFUMBASI una majina mengi sana kila kabila hapa nchini huliita wajuavyo wao kikubwa angalia picha twende pamoja. Mti huu ni miongoni mwa miti yenye sifa kubwa katika tiba, mgagani na jani la uzazi. Yote haya yanatumika katika afya hasa ya mama na mtoto. 1. Kama una maumivu wakati wa hedhi au hedhi yako haipo sawa unazdsha au kupunguza siku tafuta mti huu chemsha kisha kunywa mara tatu kwa siku. Wakati ukiwa period kunywa siku tatu mfululizo. 2. Kama una tatizo la kuharibu mimba miezi mitatu miwil na ukaambiwa tumbo lako linaunguza mimba tumia mti huu chemsha tumia kuchambia na kunywa kwa siku tatu mara tatu kwa siku. 3. Mtoto mwenye mchango mchemshie mpe kidogo anywe itatulia. 4. Tumbo linauma tu bila sababu kunywa litapoa 5. Hushiki mimba waweza chemsha kipindi unableed ukanywa siku tatu mara...
MNDEME BLOG Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, imemfutia mashtaka ya kutaka kujiua na kuamuru akapatiwe matibabu ya afya ya akili katika Taasisi ya Mirembe Isanga, mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma, Onesmo Machibya (44), maarufu kama ‘Nabii Tito’. Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kupokea ripoti za vipimo vya afya ya akili ya Nabii Tito kutoka Mirembe Isanga, vinavyothibitisha kuwa ana ugonjwa wa akili. Awali, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Kalayemaha, aliagiza kuwa Nabii Tito apelekwe katika taasisi hiyo ya magonjwa ya akili ili kupatiwa matibabu ya afya ya akili na mahakama imemwondelea mashitaka yaliyokuwa yakimkabili. Alisema katika ripoti ya kitabibu inaonyesha kuwa Nabii Tito kweli ana matatizo ya afya ya akili, hivyo anatakiwa kupelekwa katika taasisi hiyo ya Isanga Mirembe ili kupatiwa matibabu. Mahakama hiyo, Februari 5, mwaka huu, iliamuru kuwasilishwa kwa vielelezo vinavyoonesha Nabii Tito ana matatizo ya akili na kufan...
Comments