Popular posts from this blog
B R E A KING ... WAZIRI MKUU KASIM MAJILIWA KUTOA WITO..................
Waziri mkuu Majaliwa amtaka mkuuu wa mkoa wa pwani kuwasaka wafugaji wanao wapiga wakulima. Waziri mkuu Mh. Majaliwa amemtaka mkuu wa mkoa wa pwani mh Ndiklo kwasaka wafugaji wanaodaiwa kuwapiga wakulima mkoani humo. aidha waziri huyo amemtaka ndikilo kuweka kambi katika kata ya Miono mkoani pwani ili kuwapata wafugaji hao wababe. Wito huo umekuja baada ya waziri mkuu kuzungumza na wakazi wa kata ya miono wilayani bagamoyo wakati akienda kukagua miundo mbinu ya hifadhi ya taifa ya mkoani pwani. Endelea kufuatilia blog yetu ya mndeme kwa kupata habari kem kem, pia tutafute kupitia sim no. +255 652 530 530.
SUGU AHUKUMIWA KIFONGO MIEZI MITANO JELA
MNDEME BLOG Baada ya mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela, wakili wao Peter Kibatala amesema wanakusudia kukata rufaa. Sugu na Masonga wamehukumiwa adhabu hiyo leo Februari 26,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite. Wawili hao wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, kosa walilotenda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Kibatala amesema baadaye watatoa taarifa ya nini kinaendelea ila wanakusudia kukata rufaa. Baada ya hukumu kutolewa viongozi wa Chadema waliokuwepo mahakamani waliingia kwenye magari yao na kuelekea katika ofisi za chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Wakati wa usomwaji wa hukumu hiyo, nje ya jengo la mahakama ulinzi uliimarishwa kukiwa na askari waliotanda hadi maeneo...
Comments